Taasisi ya Drogba yasafishwa ‘ufisadi’; yatuhumiwa ‘kudanganya’ wahisani

0
132

Taasisi ya kusaidia watu wasiojiweza nchini Ivory Coast iliyo chini ya staa wa nchi hiyo na nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya nchi hiyo Didier Drogba imefutiwa tuhuma za kufanya ufisadi wa pesa za misaada.

Uchunguzi uliofanywa kufuatia kashfa ya kutumia £14,115 (TZS 39m) pekee kutoka kwenye msaada unaofikia £1.7m (TZS 4.7bn) baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kufanyika ufisadi au rushwa’ ingawa uchunguzi huo umedai kuwa huenda taasisi hiyo iliwapotosha wahisani.

Tume ya misaada ilianza uchunguzi wake mwezi Aprili mwaka huu kufuatia ripoti ya gazeti la Daily Maily kuwa taasisi hiyo ilifuja kiasi kikubwa cha pesa ilichopewa kama msaada kwaajili ya kuhudumia jamii za Afrika.

Drogba tayari ameshatangaza kuwa mawakili wa taasisi hiyo tayari wanatafuta haki ya kuombwa msamaha na gazeti hilo pamoja na kupewa fidia inayotokana na kuchafuliwa jina.

Hata hivyo tume hiyo imeitaka taasisi hiyo kutumia muongozo mpya wa kuboresha shughuli zake ili wahisani waweze kuelewa vizuri namna pesa wanazochangia zinavyotumika.

LEAVE A REPLY