Super Falcons watetea ubingwa wa Africa wa soka la wanawake

0
146

Kikosi cha timu ya taifa ya wanawake ya Nigeria ‘Super Falcons’ kimetwaa ubingwa wa komba la mataifa Afrika kwa wanawake baada ya kuwabamiza wenyeji Cameroon kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali.

Huku wakishuhudiwa na 40,000 jijini Yaounde, wenyeji walijikuta wakibubujikwa na machozi kufuatia goli la dakika za mwisho lililofungwa na Desire Oparanozie.

Mabingwa watetezi Nigeria wamefanikiwa kutwaa kombe hilo na kulirudisha nyumbani baada ya kulitwaa kwa mara ya kwanza mwaka 2014 nchini Namibia.

Fainali ya mwaka huu iliwakutanisha tena wapinzani waliocheza fainali mwaka 2014 nchini Namibia ambapo pia Cameroon (Indomitable Lionesses) walimaliza katika nafasi ya pili.

LEAVE A REPLY