Sumaye atema cheche kwenye kampeni za udiwani kata ya Kijichi

0
153

Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amefunguka na kusema kuwa bila kukiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani basi hali ngumu za maisha za wananchi kwa wananchi wa chini haziwezi kubadilika kamwe.

Sumaye aliyasema hayo akiwa katika uzinduzi wa kampeni za Udiwani katika Kata ya Kijichi jijini Dar es Salaam na kusema kuwa amezunguka nchi nzima na kuona jinsi watu ambavyo wanaishi katika mazingira magumu kutoka na hali ngumu ya maisha.

“Tusipoipiga CCM chini Watanzania tutaendelea kuteseka, hali ya maisha itaendelea kuwa ngumu mtapigwa maneno ya hapa na pale lakini ukweli ni kwamba bila kuwaondoa hawa watu madarakani hali za maisha ya Watanzania hazitakuja kubadilika hata siku moja, tutaendelea kupondea mitumba, miguu ya kuku na utumbo, mtaendelea kukondeana, mtaendelea kupauka na ukiona mtu amenenepa ni kwashakoo tu si afya kwa sababu maisha ni magumu” amesema Sumaye.

Sumaye amedai ili Watanzania waepukane na maisha hayo ya hovyo ambayo sasa wanaishi wanapaswa kukipiga chini Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kimeshindwa kuboresha maisha ya Watanzania toka nchi imepata uhuru mpaka leo.

 

LEAVE A REPLY