Sugu aungana na viongozi wa Chadema kuhusu uchunguzi wa shambulio la Tundu Lissu

0
126

Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema anaunga mkono hoja ya viongozi wengine wa CHADEMA kutaka serikali iruhusu vyombo binafsi vya usalama kuchunguza tukio la Tundu Lissu la kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Sugu ameandika ujumbe akisema kwamba serikali iruhusu uchunguzi kutoka vyombo binafsi vya kimataifa, ili kuwatambua na kuthibitisha waliompiga risasi Tundu Lissu.

Sumu ameandika “Nami naunga mkono kuitaka serikali iruhusu uchunguzi wa kimataifa kutoka vyombo kama FBI au ‘Scotland Yard’ ili kuwatambua na kuwathibitisha waliohusika na kitendo hiki ili wawajibishwe kwa hili jaribio la mauaji lisilo na maana, na hao wasiojulikana sasa wajulikane”.

Pia kwenye ujumbe huo Sugu ameweka wazi kuwa alitakiwa kusafiri kwenda nchini China kikazi lakini amelazimika kusitisha safari hiyo kwa sababu ya matatizo ya Tundu Lissu.

LEAVE A REPLY