Sugu afunguka kulazimishwa kuvaa sare za jela

0
323

Mbunge wa Mbeya, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema alishangazwa na kitendo cha kusikia imepigwa simu kutoka juu, na kueleza kwamba ni lazima yeye na Masonga wavae sare za jela

Akizungumzia suala hilo Sugu amesema kwamba kitendo hicho kilimshangaza kwani kulikuwa kuna watu wengine wengi walikuwa hawana sare na wamefungwa mule muda mrefu lakini walikosa sare, hivyo kitendo cha kulazimishwa yeye ambaye yuko kwa muda mfupi kilikuwa kinamshangaza.

Sugu ameendelea kwa kusema kwamba kitendo cha yeye kulazimishwa kuvaa sare hakikumkwaza kwani aliona inamsaidia kuhifadhi nguo zake.

Sugu aliachiwa huru mapema wiki iliyopita kwa msamaha wa Rais baada ya kutumikia kwa muda mfupi kifungo chake cha miezi mitano katika gereza la Ruanda mkoani Mbeya, akiwa na mwenzake Emmanuel Masonga.

LEAVE A REPLY