Sudani Kusini yaomba mkopo wa Tril. 4 China

0
108

Tovuti binafsi ya ‘Eye Radio website’ ya Sudan Kusini imeripoti taarifa ambazo hata hivyo bado hazijaripotiwa na vyombo vya serikali ya Sudani Kusini kuwa serikali ya nchi hiyo imeomba mkopo wa fedha kwa serikali ya China.

Mkopo huo unaodaiwa kulenga kutumika katika maendeleo ya nchi hiyo umeripotiwa kuwa ni $1.9bn sawa na zaidi ya trilioni 3.8 za kitanzania.

Waziri wa mambo ya nje wa Sudani Kusini, Deng Alor amesema kuwa amewashaitumia orodha ya vipaumbele vya serikali ya Sudani Kusini serikali ya China kwaajili ya tathmini.

Amesema kuwa fedha watakazopatiwa na serikali ya China zitatumika kuinua sekta muhimu ikiwemo elimu, afya na uboreshaji wa miundombinu ya usafirishaji miongoni mwa sekta zitakazonufaika.

Kwa mujibu wa Bw. Alor mpaka sasa serikali yake kupitia wizara anayoiongoza wanasubiri jibu la serikali ya China.

LEAVE A REPLY