Sudani Kusini walipinga jeshi la Afrika

0
136

Makundi mbalimbali ya asasi za kijamii na viongozi wa jadi nchini Sudani Kusini wameanza kufanya maandamano yanayoungwa mkono na serikali ya nchi hiyo kwaajili ya kupinga uamuzi wa Umoja wa Afrika wa kupeleka majeshi yake ili kusaidia kukomesha mauaji yanayoendelea nchini humo.

Maandamano hayo yanayofanyika kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Juba yanapinga uamuzi uliofikiwa kwenye mkutano wa AU uliofanyika wiki hii jijini Kigali, Rwanda ambapo ajenda ya machafuko ya Sudani Kusini iliamuliwa kwa azimio la kupeleka majeshi ya Afrika yatakayopewa mamlaka zaidi ya jeshi la Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanamalizwa.

Wanajeshi 12,000 wa Umoja wa Mataifa wapo nchini Sudani Kusini kwaajili ya kulinda amani ingawa changamoto ya machafuko imeendelea kuwepo ambapo mwanzoni mwa mwezi huu watu zaidi ya 300 waliuawa katika mapigano yaliyodumu kwa siku nne baina ya majeshi tiifu kwa rais Salva Kiir na yale yanayomtii makamu wa rais Riek Machar.

LEAVE A REPLY