Steve Nyerere ajigamba kulindwa na JB

0
78

Muigizaji wa Bongo Movie, Steve Nyerere amefunguka na kusema kuwa kwasasa analindwa na bodygud ambaye ni msanii mwenzake Jacob Steven ‘JB’.

Tukio hilo lilijiri katika Hoteli ya Hyatt Regency, Posta jijini Dar kulipokuwa na hafla ya kuzindua taasisi ya kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na bidhaa ya manukato ya De La Boss iliyoandaliwa na Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara.

Steve aliyekuwa ameongozana na JB alijigamba mbele ya watu kuwa kwa sasa analindwa naye jambo liliolofanya wengi kuangua vicheko.

Baada ya kuisha kwa shughuli hiyo, wawili hao waliongozana kutoka nje ya ukumbi huo kwa ajili ya kuondoka eneo hilo.

LEAVE A REPLY