Steve Nyerere afungukia kauli yake kuhusu Ommy Dimpoz

0
78

Muigizaji wa Bongo movie, Steve Nyerere amefunguka na kuongelea skendo inayomuandama hivi sasa dhidi ya Msanii wa Bongo movie Ommy Dimpoz.

Steve Nyerere alifanya mahojiano na kituo kimoja cha habari na kusema Ommy Dimpoz hawezi kuimba tena kwa sababu ya hali ya ugonjwa wake, huku akiwaomba Watanzania kumuombea na kuwa naye karibu ili apate faraja na kupona.

Baada ya sakata hilo Steve Nyerere ameibuka na kusema maneno hayo yanayosambazwa hayana ukweli kwani yeye hakusema hataweza kuimba kabisa bali alisema hataweza kuimba kwa wakati ule.

Ommy Dimpoz ameweka wazi kuwa ameshangazwa na kauli ya Steve Nyerere kuwa kutokana na ugonjwa Wake hatoweza kuimba hasa ukizingatia Steve hajawahi kumtafuta kumjulia hali kipindi chote alivyokuwa mgonjwa.

Ommy Dimpoz kwasasa ameachia nyimbo mpya inayokwenda kwa jina ambapo inakuwa wimbo wake wa kwanza toka apate tatizo lake hilo.

LEAVE A REPLY