Steve Nyerere achoshwa na mastaa wa Bongo Movie

0
188

Muigizaji wa Bongo Movie, Steve Nyerere amefunguka na kudai kuwa soko la filamu za Kibongo limeshuka kwasababu sura za waigizaji ni zilezile za kila siku.

Kauli ya muigizaji huyo inakuja kufuatia kipindi hiki ambacho filamu za Bongo zinaonekana kushuka na kupoteza mvuto kwa mashabiki wao hapa nchini tofauti za sinema za nje ya nchini.

Steve Steve amesema kuwa kama kila mtu anapotazama sinema anakutana na sura ya Kajala Masanja, Shamsa Ford, Aunt Ezekiel na wengine, watu wanachoka na mwisho wa siku ndipo linatokea anguko la sinema hizo.

Steve ameendelea kusema kuwa inatakiwa ufike wakati wale mastaa wakubwa waachie ngazi na kuwapa nafasi wengine ili watu waone ladha tofauti maana sura zao zimechosha mashabiki.

Filamu za Bongo zimeshuka kipindi hiki kutokana na kushuka kwa soko la filamu za ndani ambapo watanzania wameamua kujikita na filamu za nje kutokana na ubora wa filamu hizo kuliko za ndani.

LEAVE A REPLY