STEPHEN KESHI KUZIKWA LEO NIGERIA

0
104

Wapenda soka na viongozi wa michezo nchini Nigeria wamemaliza matukio maalum ya kitaifa ya kuuaga mwili wa aliyekuwa nahodha na baadae kuwa kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Super Eagles, Stephen Keshi.

Misa ya kumsalia Keshi ilifanyika jana kwenye kanisa la Mt. Paul katika mji wa kusini mwa Nigeria wa Benin.

Mechi ya hisani kwaajili ya heshima yake ilichezwa kwenye uwanja mkubwa wa mji huo huku mwili wa Keshi ukiwa umelazwa uwanjani hapo kwaajili ya heshima yake.

Siku ya Jumatano viongozi na watu maarufu kwenye soka la Nigeria wakiongozwa na waziri wa michezo wa nchi hiyo, Solomon Dalung walikusanyika kwenye mji mkuu wan chi hiyo, Abuja kufanya kumbukumbu maalum ya nyota huyo.

Keshi alikuwa nahodha wa kikosi cha Super Eagles kwa miaka 11 na amewahi kuifundisha timu ya taifa ya nchi hiyo na kufanikiwa kutwaa taji la AFCON.

Keshi amekuwa mmoja kati ya wachezaji wawili wa Nigeria kuwahi kutwaa taji la AFCON akiwa mchezaji na pia akiwa kocha.

Keshi alikutwa na mauti akiwa kwenye mji wa Benin mwezi uliopita akiwa na umri wa miama 54.

Mwili wa Keshi unatarajia kuzikwa baadae hii leo kwenye mji wa nyumbani kwao wa Illah kwenye jimbo la Delta.

LEAVE A REPLY