Stamina aachia video mpya

0
120

Msanii wa muziki wa Rap nchini, Stamina ameachia video ya wimbo wake ambao amemshirikisha Mama Mzazi wa Mwigizaji Marehemu Steven Kanumba, Bi. Flora Mutegoa.

Stamina alitangaza ujio wa video ya wimbo wake mpya uitwao Baba kupitia ukurasa wake wa Instagram, video ya wimbo ambao katika kionjo alionekana Mama Mzazi wa Mwigizaji Marehemu Steven C. Kanumba.

Kutokea kwa mama mzazi wa mwigizaji Kanumba aliyefariki mwaka 2012 kwenye video ya wimbo Baba wa Stamina inaongeza shahuku ya mashabiki kutaka kusikia mahudhui kamili ya wimbo huo ujao.

Hata hivyo wimbo huo wa Stamina utakaotoka muda wowote kuanzia sasa, umewashirikisha wakali wengine ambao ni Proffesor Jay na mwanamuziki One Six.

LEAVE A REPLY