Stamina amwagia sifa Profesa Jay

0
120

Mwanamuziki wa Hip Hop, Stamina amesema msanii na mwanasiasa Profesa Jay anatakiwa heshima ya kipekee kwani amekuwa na ushawishi kwa wasanii wengine kutokana na mchango wake kwenye muziki.

Stamina amesema hakuna msanii wa sasa ambaye hajamsikiliza Prof Jay wakati anakuwa au akijiandaa kuingia kwenye muziki pia ameipambania ‘game’ ya BongoFleva mpaka kufikia hapa.

“Prof Jay ni kaka yangu au baba ana nafasi hiyo kwangu, kuna muda nikipiga naye stori namwambia simuoni kama mpinzani ila namuona kitaifa zaidi ila tunatakiwa kuheshimu maamuzi na maisha lazima yaendelee, nimefika hadi studio za Mwanalizombe Mikumi na nina ngoma naye”

“Hakuna rapa yeyote ambaye hajawahi kumsikiliza Prof Jay, ni mmoja kati ya inspiration kubwa kwa watu pia alibadilisha akili za wazee wetu kwamba muziki sio uhuni,kwenye maisha muogope sana mtu anayepambania watu wengine”.

Prof Jay ni mmoja kati ya wasanii wa kwanza na wenye heshima kwa kuanza muziki hapa nchini Tanzania ambapo amefanikiwa kutengeneza ngoma kali ambazo zilifanya vizuri kwenye ‘chart’ na kubeba tuzo mbalimbali.

LEAVE A REPLY