Stamina afunguka ukweli wa wimbo wake mpya

0
1072

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Stamina amefunguka na kusema kuwa yote alivyoimba kwenye wimbo wake mpya ‘Asiwaze’ vimemtokea kweli kwenye maisha yake ya ndoa.

Mwanamuziki huyo amesema hayo baada ya kuulizwa kuwa je alichoimba kwenye wimbo huo kila ni cha ukweli kilichotokea kwenye ndoa yake ambapo hadi sasa wameachana na mke wake kutokana na mgogoro ndani ya ndoa yao.

Katika wimbo huo mpya ‘Asiwaze’ ameimba vitu ambavyo vimemtokea kwenye ndao yake mpaka kufikia kuachana japokuwa hakutaja sababu ya kuachana na mke wake.

Amesema kuwa “Mimi ni msanii kama kuna kitu kimenitokea najua hata kwenye jamii yangu kipo, nilichokiimba kina uhalisia kwangu na kwenye jamii, sioni mipaka mimi kama fanani kuwasilisha fasihi yangu kwa watu, hivi vitu vipo mtaani hata kama hakijanitokea mimi kuna watu vinawatokea”.

Stamina ameendelea kusema “Ukisikiliza nyimbo ambayo ipo katika historia ya kweli ya maisha, utaelewa nini ambacho kinaendelea sina haja tena ya kueleza, kama kimetokea nini au tumefanya nini na siwezi kwenda kwenye vyombo vya habari na kumuongelea mtu vibaya”.

Pia akizungumzia kuhusu mke wake kumsaliti na kutembea na aliyekuwa mchezaji wa klabu ya Simba kama alivyoimba kwenye wimbo wake, Stamina amesema “Hii ni kazi ya fasihi siwezi kusema kwamba mchezaji fulani ametoka na mke wangu, ila ninaweza nikawasilisha kitu kingine tofauti kama usaliti na sio lazima iwe hivyo kama watu wanavyofikiria”.

LEAVE A REPLY