Stamina afunguka kufumaniwa

0
84

Mwanamuziki wa Hip Hop, Stamina amefunguka na kusema kuwa hakuwahi kuwa muaminifu kwenye suala zima la mahusiano kwani alishafumaniwa mara 2 na aliyekuwa mpenzi wake.

Stamina amesema zamani alikuwa anafanya hivyo bila ya kujua thamani ya mwanamke kwa kuwa alikuwa bado hajakomaa kwenye mahusiano.

Mwanamuziki huyo ameendelea kusema kuwa “Mimi nimeshawahi kufumaniwa hapo zamani sijawahi kuwa muaminifu, nilikuwa na mwanamke mmoja ambaye nilimtesa kidogo kwa sababu sikuwa na mipango naye.

Pia ameendelea kusema kuwa mwanamke huyo alikuwa yupo serious kwake tena alifumaniwa mara 2 na mwanamke huyo huyo mmoja wakati huo alikuwa hajatulia na alikuwa haoni thamani yake”.

Stamina ni moja ya wasanii ambao walikuwa gumzo wiki kadhaa zilizopita, baada ya kuachia wimbo wake wa asiwaze, ambapo amezungumzia yaliyomtokea kwenye ndoa na alivyosalitiwa na mke wake, hali iliyopelekea kuachana kwao.

LEAVE A REPLY