Staa wa Bollywood ‘Sanjay Dutt’ awasili nchini Tanzania kwa ziara ya kitalii

0
318

Muigizaji wa Bollywood, Sanjay Dutt amewasili nchini kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii.

Sanjay Dutt  amepokelewa na Mbunge wa Jimbo la Manonga wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Seif Khamis Gulamali (CCM) kwa ajiili ya kuanza ziara hiyo.

Muigizaji huyo ameanza kutembelea na kupumzika katika mbuga ya wanyama ya Ngorongoro.

Sanjay amewahi kucheza filamu zaidi ya 100 tangu mwaka 1981 alipoanza uigizaji rasmi, hasa akibeba uhusika wa kimapenzi na uchekeshaji (komedi).

Pia Sanjay amewahi kutwaa tuzo lukuki zikiwemo  Filmfare Awards (mbili), IIFA Awards, Bollywood Movie Awards (mbili), Screen Awards (tatu), Stardust Awards (tatu), Global Indian Film Award (moja) na Bengal Film Journalist’s Association Award (moja).

Pia Filamu zake nne zilishinda vipengele mbalimbali vya National Film Awards nchini India kutokana na ubora wa kazi zake.

LEAVE A REPLY