Southgate atangazwa rasmi kuwa kocha mkuu Uingereza

0
105

Kocha wa muda wa timu ya Uingereza, Gareth Southgate ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu hiyo kwa mkataba wa miaka minne.

Southgate, anachukua mikoba iliyoachwa wazi na mtangulizi wake Sam Allardyce aliyefukuzwa kazi baada ya kudumu kwenye kibarua hicho kwa siku 67 tu.

Southgate mwenye miaka 46 ameshaisimamia timu hiyo maarufu kama THREE LIONS kwenye michezo minna na ameshinda mechi mbili na kusuluhu mechi mbili.

Mkataba wa Southgate unatajwa kuwa na thamani ya shilingi 4.5bn kwa mwaka.

LEAVE A REPLY