SOBHI WA MISRI KUJIUNGA NA STOKE CITY

0
192

Winga wa timu ya taifa ya Misri, Ramadan Sobhi anakaribia kujiunga na klabu ya ligi kuu ya Uingereza ya Stoke City.

Usajili wa mchezaji huyo umeshakamilika kwa asilimia 99 huku Sobhi akisafiri kwenda Uingereza kukamilisha uhamisho huo kutoka klabu ya Al Ahly na kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Stoke City msimu huu.

Mchezaji huyo anafuata nay za wachezaji wengine wa Misri waliowahi kucheza ligi kuu ya Uingereza akiwemo Mohamed Salah na Hossam Mido.

Staa mpya Stoke City?: Ramadan Sobhi akishangilia moja ya magoli aliyofunga
Staa mpya Stoke City?: Ramadan Sobhi akishangilia moja ya magoli aliyofunga

Ramadan Sobhi ni mchezaji chaguo la kwanza kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Misri na klabu yake ya Al Ahly licha ya umri wake mdogo wa miaka 19 tu.

Hadi sasa, Sobhi ameshafunga mabao 11 kwenye mechi 55 alizocheza kwenye timu ya Al Ahly na timu ya taifa ya Misri.

LEAVE A REPLY