Snura amwagia sifa mpenzi wake

0
173

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi amefunguka na kusema kuwa mpenzi wake, Minu Calypto amekuwa akijali sana watoto wake kuliko watu wanavyodhani.

Snura ameweka wazi hayo baada ya baadhi ya watu kdhani kuwa mwanaume huyo apende watoto wa Snura ambao amezaa na mwanaume mwingine.

Pia muigizaji huyo amesema kuwa upendo huo wa mpenzi wake umekuwa ukimpa furaha kwenye mahusiano yao kwani anajiona amepata mwanaume mwenye upendo.

Amesema kuwa “Anapenda familia yangu yaani anapenda watoto wangu na watoto wangu wanampenda sana. Tunaweza tukawa tunatoka na mtoto wangu wa mwisho akataka abaki nyumbani na mimi ndiyo nitoke,”.

Snura Mushi na Minu Calypto ni wapenzi ambao pia wanafanya muziki. Wawili hao kwasasa wametoa ngoma yao ya pamoja inayokwenda kwa jina la Shoko.

LEAVE A REPLY