Snura akanusha kutoka kimapenzi na bwana wa Nisha

0
230

Mwanamuziki na muigizaji wa Bongo Movie, Snura Mushi amekanusha kutoka kimapenzi na mpenzi wa muigizaji, Salma Jabu ‘Nisha’ aitwaye Minu na kusema kuwa jamaa
huyo ni mtu wake wa karibu tu siyo kimapenzi.

Habari hizo ziliibuka siku chache zilizopita kwenye mitandao ya kijamii baada ya msanii huyo kumtakia heri ya kuzaliwa Minu kwa maneno matamu ambayo watu walianza kujaji kuwa huenda ni wapenzi.

Baada ya taarifa hizo Snura amefunguka na kusema kuwa hana uhusiano na mwanaume huyo kwani ukaribu wao ni wa kikazi si zaidi.

“Huyo Minu siyo mpenzi wangu na wala sina muda mrefu tangu nijuane naye, kuna siku alinitafuta baada ya kupewa namba yangu na Nisha, sababu alikuwa ameandika wimbo ambao aliona nafaa kuuimba, sasa kumtakia heri ya kuzaliwa kwa kumwambia nampenda ndiyo kosa.

LEAVE A REPLY