Snura akanusha kuachana na mpenzi wake

0
212

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi ‘Snura’ amefunguka na kusema kuwa hajaachana na mpenzi wake Minu Calypto tofauti na baadhi ya watu wanavyodhani.

 Snura amesema kuwa anawashangaa watu kwa kujadili mapenzi ya watu ikiwa ya kwao yanawashinda.

Pia ameendelea na kusema kuwa “Eti mimi kuposti picha siku ya wapendanao nikiwa na mpenzi wangu, watu wakaanza kusema eti tumerudiana.

Sijawahi kuachana naye, kuhusu mimi kufuta picha zake kwenye account yangu ya Instagram ni kuamua tu lakini kwa sasa penzi letu ndio kwanza limechanua,” alisema Snura.

 

Snura alidaiwa kuachana na mpenzi wake huyo na kufuta picha zake zote Instagram, jambo ambalo lilizua mjadala mkubwa Instagram.

LEAVE A REPLY