Skyner Ally amchana Nay wa Mitego kwa kushindwa kumlea mtoto wake

0
597

Muigizaji wa Bongo Movie, Skyner Ally  amemchana msanii wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego kwa kushindwa kumuhudumia mtoto wake.

Skyner Ally amefunguka kwa kusema kuwa Nay wa Mitego ameshindwa kuwa baba bora kwa binti yake kutokana na kutomuhudumia mtoto wake aliyezaa na muigizaji huyo.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Skyaner amesema hayo wakati anamtakia heri ya kuzaliwa mtoto wake ambaye amefikisha miaka mitano na kudai kuwa alikuwa na dukuduku kutoka moyoni ndani ya miaka mitano na baada ya kuongea tayari limetoka.

“Thats face you make when you see your ‘daddy jina’ anakufanyia promotions na kudanganya watanzania kama Oooh my Twin sijui nanunua pisto, hata chupi unayovaa hajui thamani yake maskini. nimevumilia sana It’s 5 Years now nimejiskia kutapika na nimetapikaa.  Am done Mungu wa mbinguni nakuomba unijaalie maisha marefu uwezo nizidishie riziki….. uzima wa afya nikuleee mwanangu aje akuone baadae Inshallah umekuja kuwa Waziri wa nchi & Raisi wa nchi then alete pua yake”.

Pia skyner ameendelea kufunguka kuwa “Endelea na drama zako ila please shobo na mwanangu sitaki…Please unapost picha za mtoto wangu za nini…shobo dundo zanini? Sitaki shobo na mwanangu koma kama ulivyo komaaa…Je, Wababa anaojisifu kama wanapenda watoto wao then hata hawajui mtoto anakula nini anasoma wapi anavaaa nini Wapooooooo? Drama nyingi sana mtandaoni halafu i love You Nyingi Hana Analofanya Wapooooooooo ??? Am done”.

Skyner hakuishia hapo  aliendelea kutoa usia kwa binti yake kwa kuonyesha jinsi alivyo na umuhimu katika maisha ya binti yake “Hakuna anayejua thamani yako zaidi yangu hata huyo anayejita baba’ko hana analolijua kuhusu wewe, si shule, malazi wala chakula kutwa kucha kukupost na kuongopea jamii kama anakujali, ninayehangaika nimie nakuhakikishia na kumuomba Mola wangu anijaalie uhai nguvu uwezo riziki nizidi kukulea kwa nguvu zangu Inshallah nakuonea gere sana umepata mama bora na sio bora mama uko mikono salama mwanangu wa uchungu. Happy Birthday My Happiness”.

Maneno hayo makali kwa Skyner yalikuja muda mfupi baada ya Nay kuweka picha ya binti yake na kumtakia heri ya kuzaliwa na kudai kuwa amenunua bastola kwa ajili ya kumlinda.

LEAVE A REPLY