Sirro azungumza na wazee wa Kibiti na Mkuranga kuhusu mauaji

0
195

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amefanya ziara katika maeneo ya Kibiti na Mkuranga baada ya kuombwa na wazee wa maeneo hayo.

Wazee wa maeneo hayo walimataka kamanda Sirro kufuatia mauaji ambayo yamekuwa yakiripotiwa kutokea mara kwa mara.

Baada ya kuzungumza na wazee hao, IGP Sirro amesema kuwa wazee hao wametoa ushirikiano mkubwa ikiwa ni pamoja na namna ya kuwapata waharifu ambao wamekuwa wakifanya mauaji katika maeneo hayo.

Sirro amewaahidi wananchi wa maeneo hayo kuwa atatoa kiasi cha shilingi milioni 10 kwa raia mwema atakayetoa taarifa sahihi kwa watu wanaofanya mauaji mkoani.

Maeneo hao yamekumbwa na mauaji ya watu wasiokua na hatia ambapo zaidi ya watu 32 wameuawa katika Wilaya za Kibiti, Rufiji na Mkuranga mkoani Pwani.

LEAVE A REPLY