Simba yaweka kambi Zanzibar kwa ajili ya mechi dhidi ya Yanga

0
518

Simba SC inaendelea na kambi yake visiwani Zanzibar ikijiandaa na mchezo dhidi Yanga Februari 25 ya Jumamosi wiki ijayo.

Nahodha wa Simba, Jonas Mkude amesema kwamba hadi sasa wako vizuri kuelekea mchezo huo wa Februari 25.

Simba imekwenda kambini Zanzibar siku moja baada ya kutinga Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kufuatia kuifunga 1-0 African Lyonjuzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, bao pekee la Laudit Mavugo.

Kikosi cha Simba kilichoingia kambini hapo jana kinaundwa na

Makipa; Daniel Agyei, Peter Manyika na Dennis Richard.
Mabeki: Janvier Bokungu, Hamad Juma, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdi Banda, Vincent Costa, Novaty Lufunga na Method Mwanjali.

Viungo: Jonas Mkude, James Kotei, Said Ndemla, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim, Muzamil Yassin, Mwinyi Kazimoto, Shiza Kichuya na Jamal Mnyate.

Washambuliaji: Laudit Mavugo, Pastory Athanas, Ibrahim Ajibu, Hijja Ugando na Juma Luizio.

 

LEAVE A REPLY