Simba yaanza mazoezi kujiandaa na Mbao

0
231

Klabu ya soka ya Simba imeanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo wake wa kiporo raundi ya 19 ligi kuu dhidi ya Mbao FC ya Mwanza.

Baada ya kurejea nchini jana ikitokea Djibouti kwenye mchezo wake wa marudiano dhidi ya Gendarmerie, benchi la ufundi la klabu hiyo lilitoa mapumziko ya siku moja kwa wachezaji.

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo, mazoezi yanatarajiwa kuanza leo saa 10:00 jioni katika uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam.

Simba imefanikiwa kutinga hatua ya kwanza ya michuano ya kombe la shirikisho baada ya kuitoa Gendarmerie kwa jumla ya mabao 5-0 na inatarajiwa kukutana na Al Masry ya Misri.

Simba inaongoza msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara ikiwa na alama 42, ikiwazidi wapinzani wao Yanga wenye alama 37 katika nafasi ya pili huku Azam FC ikiwa katika nafasi ya tatu na alama 35.

LEAVE A REPLY