Simba wamtangaza kocha mpya wa klabu hiyo

0
199

Klabu ya Simba leo imemtangaza kocha mpya wa klabu hiyo Pierre Lechantre kuchukua nafasi ya Joseph Omog aliyetimuliwa.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Klabu hiyo, Haji Manara imeeleza kuwa kocha huyo ataanza kazi mara moja na atasaidiwa na kocha msaidizi wa sasa Masoud Djuma .

Kocha huyo mpya atashuhudia mchezo wa Simba SC dhidi ya Singida United leo Januari 18, 2018 katika Uwanja wa Taifa.

Pierre Lechantre alishawahi kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Cameroun kilichoshinda ubingwa wa Afrika mwaka 2000 na ameshawahi kushinda tuzo ya kocha bora wa bara la Afrika 2001.

LEAVE A REPLY