Simba kumpokea Okwi kesho jijini Dar es Salaam

0
273

Klabu ya Simba imesema kuwa kesho Jumamosi itampokea straika wao wa zamani, Emmanuel Okwi, tayari kwa kumpa mkataba wa miaka miwili ya kuitumikia timu hiyo.

 Okwi ambaye aliwahi kuitumikia Simba kwa vipindi viwili tofauti anajiunga tena na timu hiyo akitoke SC Villa ya nyumbani kwao ambayo alikuwa akiichezea mara baada ya kuachana na SonderjyskE ya Denmark.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, hivi karibuni alikuwa jijini Kampala, Uganda kwa shughuli zake binafsi ambapo alitumia mwanya huo kumalizana na Okwi.

Hanspop amesema kuwa “Nilienda Kampala katika mkutano wa mambo tofauti na soka, nikiwa kule nikaona mtandaoni kuna picha inasambaa kwamba eti Okwi ameingia Dar, picha hiyo ilimuonyesha akiwa amevaa kofia, sasa wakati naiona ile picha nilikuwa karibu na Okwi, nikaona bora niwaumbue watu waongo, tukapiga picha, nikazituma.

 “Sasa watu wakabadilisha mada, wakaanza kuzungumza kwamba tushamalizana naye wakati mimi nilitupia picha tu bila ya kuandika chochote.

Ameongeza kwa kusema kuwa “Okwi ana uwezo wa kubadilisha matokeo muda wowote, tumekuwa tukimfuatilia tangu awe anacheza soka Uganda na tumeona bado ni mchezaji mzuri, kitendo cha kufunga mabao saba kwenye mechi saba kimedhihirisha hilo.”

LEAVE A REPLY