Shule zilizoathiriwa na tetemeko la ardhi kujengwa tena upya

0
171

Serikali imeahidi kuzijenga upya shule zote zilizoharibiwa vibaya na tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni mkoani Kagera na kutoa siku tatu kwa maafisa elimu mkoani humo kuwasilisha takwimu sahihi.

Hayo yamesemwa na waziri wa elimu, sayansi na teknologia, Profesa Joyce Ndalichako alipotembelea shule zilizoathiriwa vibaya.

Amesema serikali ipo tayari kujenga upya shule zilizoharibika vibaya na tetemeko hilo, huku akiwataka walimu wakuu kufanya ukarabati katika shule zilizoathiriwa kwa kiasi kidogo.

Waziri Ndalichako amesema “Nachoweza kusema madhara yanatofautiana,kuna shule zingine zimeathirika ufa ambao wanaweza wakaangalia, hata zile fedha tunazotoa za elimu bure inaweza ikatumika, kwasababu kuna components ya ukarabati,kwahiyo kuna sehemu nyingine wanahitaji mifuko miwili mitatu ya simenti unarekebisha. Lakini kuna shule nyingine ambazo unakuta ufa ni mkubwa, na unakuta ukuta mzima inabidi kuubomoa,”.

Profesa Ndalichako alisema shule zilizoathirika ni pamoja na Ihungo. “Yaani hii shule nzima ukiangalia madarasa, mabweni, nyumba za walimu kwa maana nyingine inatakiwa kujengwa upya,”.

LEAVE A REPLY