Should we learn or should we complain?

0
106

Wasanii wa Tanzania wamekuwa (kwa miaka mingi) wakifanya jitihada kubwa sana ya kuhakikisha kuwa kazi zao zinafika kwenye nchi za nje ili nao waweze kutambulika kimataifa.

Juhudi hizo zinajumuisha mbali ya mambo mengine lakini pia kutengeneza video zenye maudhui ya muziki wa nje, mitindo ya maisha nakadhalika ambayo yote ni kutoka nje ya mipaka ya Tanzania na wakati mwingine hata nje ya miapaka ya Afrika.

Jitihada nyingine imekuwa ni kuwashirikisha (kwenye kazi zao) wasanii kutoka mataifa hayo (ambapo wasanii wa Tanzania wanatamani kazi zao zichezwe), na inapotokea kazi za wasanii wetu zinapochezwa kwenye vituo vikubwa, hiyo huwa ndio stori kubwa kwenye mitandao ya kijamii……Wow!!

Lakini msanii wa kitanzania mwenye makazi yake nchini, Sweden, The Dati amekuja na sababu ‘genuine’, kwanini (licha ya jitihada zote wanazofanya wasanii wetu bado kazi zao hazichezwi kwenye nchi kubwa).

Vyombo vya habari vya kimataifa vinaheshimu au kuogopa sheria za haki miliki hivyo licha ya kujali uzuri wa kazi ya msanii na hamu ya msanii na mashabiki wake kutamani kazi hiyo ichezwe huko bado vyombo hivyo vinahitaji mkataba wa makubaliano ya kuchezwa kwa kazi hiyo na malipo kwa mmiliki wa kazi hiyo.

kiba

Je, wasanii wa Bongo, lipi mnataka? Kazi zisichezwe mpaka muingie kwenye mikataba na vyombo hivyo (ambayo itaeleza malipo yenu) au mko tayari kazi zenu zichezwe ili tu ‘mjulikane’ Ulaya na mashabiki wenu wazidishe kutambiana kwenyesocial media kuhusu msanii gani kazi yake imechezwa zaidi na vituo vingi n.k?

Ni wakati wa wasanii wa Bongo kuamua; KUJIFUNZA au KULAUMU, chagua moja!

LEAVE A REPLY