Shomadjozi apata dili nchini Marekani

0
73

Msanii wa muziki kutoka nchini Afrika Kusini, Maya Christinah Xichavo Wegerif maarufu zaidi kama Shomadjozi amesainiwa na lebo maarufu ya muziki ya nchini Marekani, Epic Records.

Shomadjozi aliyetamba zaidi na wimbo wake ‘John Cena’ alisaini na lebo hiyo kongwe ambayo ni kampuni inayofanya kazi nchini ya Sony Music Entertainment.

Mwanamuziki huyo amebainisha hayo kupitia ujumbe aliouweka kwenye mtandao wake wa twitter kubainisha taarifa hizo za dili lake.

Shomadjozi baada ya mkataba wake huo na Epic, ameingia kwenye orodha ya wakali wengine maarufu Duniani chini ya lebo hiyo kama vile, DJ Khaled, Maria Carey, Rick Ross, T.I, Camila Cabello na wengine kibao.

Mwanamuziki huyo kwasasa anaendelea kufanya vizuri nchini Afrika Kusini kutokana na nyimbo zake zinazotamba nchini humo mpaka kupelekea kubata dili hilo.

LEAVE A REPLY