Shilole: Ndoa siyo jela

0
29

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole baada ya kupitia mgogoro na mumewe Ashraf Uchebe amesema kuwa ndoa siyo jela, kama kitu ukishindwa unaondoka tu.

Shilole amesema kuwa, ndoa nyingi zinapitia migogoro si kwake tu, hata mtu akishindwa anaenda tu.

“Unajua mambo ambayo nimepitia si mimi tu, ni ndoa nyingi zinapitia haya mambo ya migogoro, hivyo usione kitu cha ajabu, kama ukiona mambo magumu, unaondoka tu maana ndoa siyo jela,’’ alisema Shilole.

Shilole ambaye pia ni muigizaji wa Bongo Movie amesema kuwa kama mwanaume akujali na anakupiga kila wakati ni vyema kuachana nae kwani anaweza kukusababishia matatizo.

Shilole aliacha na mume wake hivi karibuni baada ya kushushiwa kipigo na kumsababishia maumivu makali kiasi cha kulazwa kutokana na kipigo hicho.

LEAVE A REPLY