Shilole awatahadharisha wanaomtaka Uchebe

0
54

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amewajia juu na kuwatolea uvivu wanawake wanaomuwinda Mume Wake wa ndoa Uchebe.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Shilole amevunja ukimya, awatolea uvivu wanawake wanaomuwinda mume wake akisisitiza ametumia nguvu kubwa kumpa mwonekano alionao sasa.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa aliridhika na hali yake tangu mwanzo mpaka sasa anashaini ila wadangaji wanamtolea macho mpenzi wake.

Shilole alifunga ndoa na Uchebe Desemba ya mwaka 2017 na Uchebe ambaye ni fundi gereji na asiyejulikana lakini tangu ameanza mapenzi na Shilole ameonekana kunawiri na hivi sasa anaishi maisha ya kifahari na msanii huyo.

Wawili hao bado hawajafanikiwa kuwa kupata mtoto toka wafunge ndoa lakini mwanamuziki huyo amesema kuwa yupo mbioni ya kumzalia mume wake huyo.

LEAVE A REPLY