Shilole awashukuru waandaaji wa tuzo za Malkia wa Nguvu

0
185

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole amewashukuru waandaji wa tuzo za malkia wa nguvu baada ya kumuwezesha kushinda tuzo kwenye hafla iliyofanyika siku ya Jumamosi jijini Dar es Salaam.

Shilole ameshinda tuzo hiyo kwenye kipengele cha mfanyabiashara bora wa chakula akiwa kama mjasiliamali kwenye upande wake wa uuzaji wa chakula.

Mwanamuziki huyo ana miliki mgahawa wa Chakula maarufu kama Shishi Food ambapo usambaza chakula kwa wateja wake waliopo jijini Dar es Salaam.

Pia Shilole amesema kuwa kwake tuzo hiyo ni kitu kikubwa sana kwani inamtia nguvu ili kuendelea kufanya vitu vikubwa sana kwenye kazi yake hiyo upishi.

Vile vile amewashukuru waandaji wa tuzo hizo Clouds Media kwa kutambua mchango wa wanawake hapa nchini kwa kuwatia moyo ili kufikia ndoto zao.

Tuzo za Malkia wa nguvu uandaliwa na kampuni ya Clouds Media Group na ufanyika kila mwaka jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutambua mchango wa wanawake katika jamii.

LEAVE A REPLY