Shilole awapa makavu wasanii wenzake

0
97

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole ameibuka na kuwajia juu wasanii ambao wameonekana kusapoti na kulilia wasanii wenzao Baada ya kifo.

Siku ya jana Msanii wa muziki wa hip hop nchini Godzillah alifariki dunia Baada ya kuugua ghafla nyumbani kwake Salasala. Wasanii mbali mbali walijitokeza kutoa pole na hata kumposti katika kurasa zao ya Mitandao ya kijamii.

Shilole amewajia juu baadhi ya wasanii ambao amediriki kuwaita wanafki na kudai wamejitokeza Baada ya kifo chake na kuanza kumposti na kudai wameguswa wakati kwenye uhai wake hakuna hata mmoja aliyeposti kazi zake.

Mimi naona ni vizuri mtu akapewa heshima yake wakati yuko hai ili aone kama kuna watu wanampenda na kumjali sasa leo hii amekufa ndio anapewa hiyo sapoti.

Wakati yupo hai anatoa nyimbo hamposti wengine mpaka wanatumia ngoma zake kama cover lakini bado hawamposti wala kumpa heshima yake kama legendari ndio maana  mimi kila siku nasema wasanii tuache unafiki wengi watu ni wanafiki sana”.

LEAVE A REPLY