Shilole amwagia sifa mpenzi mpya wa Diamond

0
257

Mwanamuziki wa Bongo Fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole ameibuka na kuwamwagia sifa kibao staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Mpenzi wake Tanasha Donna.

Siku za nyuma Shilole hakuficha hisia zake za Jinsi gani alikuwa anamkubali Mama watoto wa Diamond, Zari na hata kumuomba Diamond arudiane naye Baada ya kuachana.

Lakini Hivi sasa Zari anaoenekana kumsahau Zari na kuhamisha majeshi yake kwa wifi yake Mpya Tanasha kwani ameshindwa kujizuia na kumwagia sifa kibao mrembo huyo.

Shilole ameweka wazi kuwa Tanasha anapendezana na Diamond na hata kudai tangu amekuwa naye amekuwa akipendeza zaidi hasa Baada ya kunyoa.

Diamond na Tanasha wanapendezana sana, siku hizi naona hata Diamond ananyoa vizuri kusema Ukweli wapo kizazi sana”.

Stori za chini chini zinadai kuwa Shilole alikoromewa na Diamond Baada ya kumtaka arudiane na Zari kwenye mkutano na waandishi wa habari Wiki chache zilizopita.

LEAVE A REPLY