Shilole akanusha kugombana na mume wake Uchebe

0
157

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole amesema kuwa hawezi kupigana na mume wake Uchebe kwani mapenzi ya kupigana ni ya utoto.

Shilole amefunguka hayo baada ya kuzoeleka na watu wengi kwa tabia yake ya kupiga wanaume ambao anakuwa nao katika mahusiano.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa kwasasa hawezi kuthubutu kufanya hivyo na kama atampiga mume wake basi ni wakiwa faragha tu.

Shilole amesema kuwa hawezi kupigana na mume wake maana alikuwa anapigana ngumi kabla ya kuwa yeye na ana mkanda wa karate.

Pia Shilole ameendelea kwa kusema yeye ni mtu makini sana anaejitambua na kujithamini hivyo hawezi kupigana na mume wake.

LEAVE A REPLY