Shilole akanusha kuachana na Uchebe

0
242

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole amekanusha taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii za kuachana na mume wake Uchebe.

Shilole amesema kuwa hajaachana na mume wake na wala hawafikirii kuachana ila matatizo ni kawaida kwenye mahusiano.

Kwa upande wa Uchebe amesema sio kweli kwamba ameachana na mkewe, na kwamba kuna wanafiki wanapenda wasikie wameachana.

Akifunguka kuhusu kupost kwa ua jeusi na caption yenye utata, Uchebe amesema kuna mtu alihack acount yake na kupost hivyo, lakini hawajaachana namkewe na wala sio kiki.

Tetesi za wawili hao kuachana zimekuja baada ya kupostiwa kwa ua jeusi kwenye ukurasa wa instagram wa Uchebe na caption ambayo ilikuwa na utata, na watu kuhisi labda wawili hao hawako pamoja tena.

LEAVE A REPLY