Shilole afurahia penzi lake jipya

0
10

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole amesema kuwa kwa sasa ametulia tuli kwenye penzi lake jipya na Rommy3D baada ya kuachana na Uchebe.

 

Shilole amesema kuwa laiti angejua kuwa angekuja kukutana tena na mpenzi wake huyo wa muda mrefu, angekaa na kumsubiri asingepita kwenye mikono ya wanaume waliompiga danadana.

 

Amesema kuwa Naomba nikiri kwamba Rommy amenifanya nijione mpya tena kwa mara nyingine, laiti ningejua kama angerudi tena kwenye maisha yangu ningekaa na kutulia kumsubiri.

 

Wala nisingehangaika na wanaume wasiojua thamani ya mwanamke hata kama ulimwengu upinduke sitapepesa macho kuchangua ila nitamchagua yeye,” alisema Shilole.

 

Shilole na Rommy walikuwa wapenzi miaka mingi iliyopita kisha kila mmoja alishika njia yake kabla ya kufufua penzi lao hivi karibuni.

LEAVE A REPLY