Shilole afunguka kupigwa na Uchebe

0
226

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole amefunguka na kuelezea kichapo kizito alichotembezewa na mumewe Uchebe ambapo amedai kisa na mkasa ni yeye kucheza mziki na Soudy Brown kwenye sherehe.

Soudy Brown alifunguka kuwa alipokea taarifa kuwa Shilole alipokea kichapo kizito kutoka kwa mumewe Uchebe baada ya kurudi nyumbani usiku wa manane akitokea kwenye party Tabata.

Pia Shilole alikiri kupigwa kama mtoto na Uchebe kiasi kuwa walifunga mtaa hadi kupelekea Shilole kwenda kulala kwa marafiki zake.

Yaani Uchebe amenipiga kama mtoto mdogo lakini haina noma mimi mwanamke na dunia nzima inajua mimi mwanamke kuna mambo mimi nitakuja kusema mazito alafu ndo nitakapodai Talaka yangu.

Taarifa za kuachana kwa wawili hao zimezagaa katika mitandao ya kijamii baada kuripotiwa na watu wake karibu kuhusu.

LEAVE A REPLY