Shilole afikiria kuandika kitabu chake

0
23

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mjasiriamali Shilole amekuja na wazo la kuandika kitabu kitakachosimulia maisha yake hadi hapo alipofikia.

Shilole amehabarisha hilo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ambapo ameandika kuwa

“Nafikiria kuandika kitabu, nafikiria kuacha alama, nafikiria kuelezea mapito na magumu yaliyonijenga leo hii kuwa Shishi,  haikuwa rahisi hata kidogo lakini pia hakuna gumu unapoamua kutokukata tamaa, kuweka juhudi, kumumuweka Mungu mbele na kuzikimbiza ndoto zako”

Shilole ni mmoja wa watu maarufu na wenye ushawishi kwa wanawake wengi kwa sasa kuanzia kazi na biashara zake kutokana na mafanikio aliyoyapata na vitu ambavyo amepitia kama kubakwa, kupata watoto akiwa na umri mdogo,

Kubezwa kwenye filamu na muziki, na kubwa zaidi kupigwa na aliyekuwa mume wake Ashraf Uchebe.

LEAVE A REPLY