Shilole aanzisha lebo ya muziki

0
52

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole ambaye pia ni muigiza wa Bongo movie ameanzisha lebo ya muziki iitwayo Shish Gang ambayo itakuwa inasimamia wasanii na kuwatowa wasanii wapya.

Shilole ameeleza kuwa lebo hiyo itakuwa inafanya mambo mengi na sio muziki tu pamoja na shughuli nyingine zinazohusiana na burudani hapa nchini.

Pia ameongeza kuwa katika lebo hiyo Baba Levo ndio msemaji wake ingawa hakuwepo “Hata msanii wake atamsaini kwenye lebo hiyo kwani wapo kwenye mazungumzo.

Kwa upande mwingine Shilole ameongeza kuhusu kufanya collabo na wasanii wa Afrika Wiz Kid pamoja na Koffi Olomide ambao tayari ameshafanya nao mazungumzo kuhusu kolabo hizo.

Shilole ameongeza kuwa ingawa alipata shida sana kuongea na uongozi wa Wiz Kid lakini kwa sababu meneja wa Wiz Kid Sunday anamkubali sana hivyo wameelewana atasafiri kwenda Nigeria kwa ajili ya kurekodi.

Kuhusu Collabo na Koffi Olomode amesema kuwa mipango tayari imekamilika na pia atasafiri kwenda Congo kwa ajili ya kurekodi kwenye studio ya Koffi jijini Kinshasa.

LEAVE A REPLY