Sheria ya Trump ‘Chaliii’, jaji aongeza muda zaidi wa zuio la kusafiri

0
162

Jaji wa mahakama kuu ya jimbo la Hawaii nchini Marekani ameongeza muda wa kupinga zuio la kusafiri kwa raia kutoka baadhi ya mataifa lililowekwa na rais wa Marekani Donald Trump.

Kutokana na hukumu hiyo ya Jaji, Derrick Watson rais Trump hawezi kufanikisha azma yake ya kuzuia raia wa mataifa ya Iran, Libya, Somalia, Sudan na Yemen kuingia na kutoka Marekani wakati shauri hilo lilikiwa linasikilizwa mahakama kuu.

Kwenye kesi ya msingi, jimbo la Hawaii limedai kuwa sheria hiyo itaathiri utalii na kuzuia uwezo wa kudahili wanafunzi wa elimu ya juu kutoka mataifa mengine pamoja na kupata wafanyakazi kutoka mataifa hayo.

Rais Trump alidai kuwa katazo la mara ya pili la kuruhusu uingiaji na utokaji wa raia wa nchi hizo ndani ya Marekani umelenga kuzuia magaidi kuinia nchini humo.

LEAVE A REPLY