Shamsa Ford kumpeleka mzazi mwenzake kwa Makonda

0
353

Muigizaji wa Bongo Movie, Shamsa Ford amesema kuwa atampeleka mzazi mwenzie Dickson Matoke Kwa RC Makonda kwa ajili ya kudai haki ya kuhudumiwa mtoto wake.

Shamsa alisema kuwa sio kwamba hana uwezo wa kumhudumia mtoto wake lakini kuna wakati unaumia kuona baba wa mtoto yupo, anakula bata tu akiwa hajui hata kula ya mtoto wake inatoka wapi.

“Dawa ya wanaume wa sampuli hii ni kuwapeleka tu kwa Makonda. Mimi watu watashangaa sana siku watakaponiona pale lakini ni kwa sababu wakati mwingine ukifikiria unajikuta unapatwa na hasira kuona mzazi yupo lakini kama hayupo vile,” alisema Shamsa.

Jumatatu iliyopita, akinamama wengi waliotelekezewa watoto wamekuwa wakifika kwa Makonda ili kusaidiwa lakini hakuna staa wa kike aliyetinga hadi juzi Alhamis.

LEAVE A REPLY