Shamsa Ford awachana wanaomsema kuhusu kupata mtoto

0
76

Muigizaji wa Bongo Movie, Shamsa Ford amesema kuwa  kwamba ndoa si mtoto na kila mtu ana mipango yake ya kuzaa baada ya ndoa, hivyo waache kuongea wasiyoyajua.

Shamsa amesema kila ndoa ina mipango haswa katika suala la kupata mtoto kuna wengine wanapanga kuzaa hata baada ya miaka mitano hivyo hata yeye na mume wake wana mipango yao ya ndani ya ndoa hivyo pale mwenyezi mungu atakapowabariki watapata mtoto.

“Kikubwa ambacho naweza kuwaambia watu ni kwamba tuombeane mema kwa kuwa maisha ni mafupi na hakuna anayeujua mwisho wake na hata katika dini Mungu amesema kwamba ukimuombea mwezio mema na wewe utabarikiwa zaidi”, amesema Shamsa.

“Hivyo kama kuna mtu ambaye hajaolewa na ananiombea mimi niachane na mume wangu basi ni bora awe makini kwa kuwa yeye anaweza akakosa hata mume wa kumuoa kwa kuniombea mimi mabaya”.

Hata hivyo Shamsa alimalizia kwa kusema kwamba siku ya harusi yao kuna watu walidhani kwamba ataachana na Chid baada ya muda mfupi lakini kwa uwezo wa Mungu mpaka sasa ni mwaka wa tatu.

LEAVE A REPLY