Shamsa Ford atulia nyumbani kisa Corona

0
226

Muigizaji wa Bongo Movie, Shamsa Ford amesema kuwa ugonjwa wa Covid19 umemfanya atulie nyumbani tofauti na hapo awali kwa kuhofia kuambukizwa ugonjwa huo.

Shamsa Ford amesema kuwa ugonjwa huo ni tishio sana hivyo amepunguza safari ambazo hazina umuhimu tofauti na hapo kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa huo ambao umeua maelfu ya watu dunia kote.

Shamsa alisema kuwa kwa sasa ametulia tu nyumbani mpaka hapo hali itakapokuwa sawa hata biashara zake za madera ameacha kwa hofu ya ugonjwa huo unaosababishwa na virusi vya Corona.

“Nilizoea muda mwingine kutoka tu ili kwenda kupoteza mawazo, nilikuwa naweza kwenda beach au hata nje ya nchi ili mradi nikale bata tu, lakini kwa sasa sitoki mpaka hili janga liishe.

Yaani hapa hamna namna, lazima tujilinde sisi na familia zetu ili uishe maana ukiisha tutaendelea kula bata kama zamani, kikubwa ni kuvumilia tu,” alisema Shamsa.

Kutokana na maambukizi ya ugonjwa huo hapa nchini Serikali imesimamisha shughuli zote zinazokutanisha watu wengi ili kuepuka kusambaa kwa ugonjwa huo.

LEAVE A REPLY