Shamsa Ford atamani kuolewa tena

0
41

Muigizaji wa Bongo Movie, Shamsa Ford amefunguka na kusema kuwa anatamani kuolewa tena baada ya kushuhudia muigizaji mwenzake Elizabeth Michael kufunga ndoa na Majizo.

Shamsa ameandika” ”Umepitia mengi ya kukuumiza mdogo wangu Elizabeth, umevumilia mno maneno ya waja hatimaye leo unafurahi.

“Tabasamu mama na tabasamu la kudumu milele Inshaallah, Mungu aitangulie ndoa yako iwe ya furaha na amani tele mdogo wangu.

“Hongera my kaka Majizo wewe ni mfano bora wa kuigwa na vijana wengine hakika una mapenzi ya dhati  na uvumilivu, hukukata tamaa na changamoto zozote mpaka hii siku imefika Mungu ni mwema ,umenitamanisha kuolewa tena,” ameandika Shamsa.

Shamsa mwaka 2016 alifunga ndoa na mfanyabiashara Chid mapenzi ndoa ambayo hata hivyo ilikuja kuvunjika mwaka 2019.

LEAVE A REPLY