Shamsa Ford ataki tena ndoa

0
16

Muigizaji wa Bongo Movie, Shamsa Ford amesema kuwa ana muda mrefu wa kula ujana bila kuwa na mwanaume yeyote wa kuishi naye ndani mpaka atakapoona ametosheka vilivyo ndipo atafikiria jambo hilo.

Shamsa amesema kuna wakati wanawake wanakuwa hawajamaliza kula ujana wao vizuri na badala yake wakiingia kwenye ndoa moja haikai wala mbili haikai na mwisho wa siku ndoa inavunjika hivyo ni bora kumaliza ujana kwanza.

“Wanawake wengi hawajui, wanakimbilia kuingia kwenye ndoa mapema lakini baada ya muda ndoa inakufa maana bado wanatamani sana mambo ya nje na hata mimi nimejifunza sasa nakula ujana kwanza mpaka nitosheke.

Ameendelea kusema kuwa baada ya miaka kumi mbele ndio nitaingia tena kwenye ndoa rasmi baada ya kuona sasa nimeshamaliza masuala ya ujana.

Shamsa alikuwa kwenye ndoa na mfanyabiashara wa maduka ya nguo nchini Chini Mapenzi ambapo kwasasa wameachana toka mwaka jana.

LEAVE A REPLY