Shamsa Ford apigwa marufuku na mumewe kutumia mitandao

0
449

Muigizaji wa Bongo Movie, Shamsa Ford amefunguka na kuthibitisha kuwa mume wake alimwambai aache kutumia mtandao wa kijamii hasa instagram ili kuepusha shari na matusi kutoka kwa mashabiki.

Shamsa Ford ambae kwa sasa amekua haonekani sana katika mitandao ya kijamii  huku sababu ikisemekana kuwa sababu ni kukatazwa na mume wake chid mapenzi.

Mtu wa karibu na Shamsa Ford alisema kuwa shamsa alikatazwa kutumia mitandoa hiyo kwa sababu alikuwa akitumia muda mwingi katika mtandao wa instagram.

Shamsa Ford na chid mapenzi ni moja ya couple ya watu maarufu walioweza kufunga ndoa na kudumu bila kuwa na skendo wala maneno ya hapa na pale kuhusu ndoa yao, ilhali inafika muda mpaka Shamsa anatumia muda wake kuwashauri wanawake wengien kuingiakatika ndoa na jinsi ya kuishi na mume vizuri.

Madhaifu mengi ya wasanii yamekuwa yakionekana kupitia mitandoa na wamekuwa wakikumbana na matusi mengi katika mitandao hiyo.

Muda mwingine kwa kujua au kutokujua mashabki hujikuta wakimu-attack msanii na kumtukana bila kujua sababu ya vitu vinavyotokea

LEAVE A REPLY