Shamsa Ford amtahadharisha Wema Sepetu kuhusu tabia ya kuhama hama vyama

0
111

Baada ya muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu kuhama chama kutoka Chadema kwenda CCM, msanii mwenzake Shamsa Ford amemtahadharisha muigizaji huyo kuhusu tabia hiyo.

Muigizaji huyo amemtaka Wema kuacha tabia ya kuhama chama kwasababu anaweza kupoteza mashabiki kutokana na kitendo chake hicho.

Shamsa amesema wao siyo wanasiasa hivyo suala la Wema la kwenda na kurudi kwenye vyama vya siasa inawezekana anapata faida lakini cha muhimu asisahau kazi yake.

Amesema kuwa “Siwezi kuzungumzia sana suala la Wema kuhama vyama maana ni lake binafsi na huenda lina faida kwake, nawasihi tu wenzangu wasisahau kazi yao ya sanaa iliyowatambulisha kwa jamii,”.

Wema Sepetu wiki iliyopita alitangaza kukihama Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kurudi CCM alipokuwa hapo awali.

LEAVE A REPLY