Shamsa Ford akiri kuachana na mumewe

0
650

Baada ya kusambaa kwa taarifa nyingi kuhusu ndoa yake mitandaoni, hatimaye mrembo kutoka Bongo Movie, Shamsa Ford amekiri kumwagana na mumewe Rashid Said maarufu kama ‘Chid Mapenzi’.

 

Taarifa za Shamsa kumwagana na mumewe zilianza kusambaa katikati ya wiki hii ambapo kwenye mitandao ya kijamii hususan Instagram, kila mmoja alisema lake.

 

Kuna ambao walisema ni kweli wameachana lakini kuna wengine walisema taarifa hizo hazina ukweli wowote licha ya kusambaa katika mitandao ya kijamii.

 

Mwingine akasema: “jamani mimi kuna mtu yupo karibu sana na Shamsa kanimegea kabisa kwamba ndoa yao imeshaota mbawa.”

 

Muigizaji huyo amekiri kuachana na mumewe lakini hakuwa tayari kuzungumzia zaidi suala hilo kwakuwa kila kitu kitajulikana hapo baadae.

LEAVE A REPLY